Pata taarifa kuu
CAIRO-MISRI

Kundi la wapiganaji linalosakwa Misri lamuua askari polisi

Afisa polisi ameuawa kwa risasi jijini Cairo nchini Misri katika harakati za kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya Afisa usalama,wizara ya mambo ya ndani imearifu.

Mmoja kati ya wapiganaji wa Ansar Beit al-Maqdis mjini Cairo ,ambao wanamahusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda
Mmoja kati ya wapiganaji wa Ansar Beit al-Maqdis mjini Cairo ,ambao wanamahusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda beforeitsnews.com
Matangazo ya kibiashara

Askari huyo aliyejulikana kwa jina la Ahmed Samer Mahmoud aliuawa alfajiri ya alhamisi huko Nile Delta baada ya kufika na kikosi maalum na kushambuliana na kikundi cha watu wenye silaha.

Kikundi hicho cha wapiganaji kinasakwa kwa kuhusika na mauaji ya luteni kanali Mohamed Mabruk, ambapo taarifa ya wizara imeeleza watuhumiwa wawili wamefanikiwa kutiwa mbaroni.

Mabruk,afisa ambaye alishiriki operesheni dhidi ya ghasia zilizosababishwa na waislamu na wafuasi wa raisi aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi alipigwa risasi na kufa papo hapo siku ya jumapili.

Kikundi cha wapiganaji chenye makazi yake Sinai na kudaiwa kujihusisha na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Ansar Beit al-Maqdis,kilidai kutekeleza mauaji hayo.

Wapiganaji hao wakiwemo Ansar Beit al-Maqdis wamekuwa wakifanya mashambulizi tangu kupinduliwa madarakani kwa raisi Morsi na wameongeza kulenga mashambulizi katika ofisi za wanausalama.

Kundi hilo pia awali liliwahi kudai kuhusika na ulipuaji wa ofisi ya mjumbe wa waziri wa mambo ya ndani shambulizi ambalo lilishindwa kutimiza azma yao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.