Pata taarifa kuu
SOMALIA

Takribani watu 16 wamekufa katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab nchini Somalia

Takribani watu 16 wamepoteza maisha leo jumanne kufuatia shambulizi lililotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab katika kituo cha polisi mjini Beledweyne nchini Somalia. Kwa mujibu wa mashuhuda ni kuwa mwanachama mwanachama mmoja wa kundi hilo alijitoa mhanga kwa kujilipua kwenye gari katika lango la kuingilia kituoni hapo kabla ya Makomandoo wengine kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwamo ndani.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab ameliita shambulizi hilo ni ushindi dhidi ya vikosi vya usalama vinavyoshiriki oparesheni ya kuwatokomeza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi nchini humo, Abdi Mohamed Ali waliouawa ni wanajeshi na wengine ni raia wa kawaida. Aidha amethibitisha kuwa polisi wamefanikiwa kuwaua watu wanne ambao ni wanachama wa Al Shabaab.

Naye kiongozi wa Al Shabaab, Kamanda Sheikh Mohamed Abu Suleiman ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa shambulio hilo liliwalenga maadui zao ambao ni wanajeshi wa Ethiopia, Somalia na Djibout wanaoshirikiana na vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM.

Mwezi uliopita shambulio jingine lilisababisha vifo vya watu takribani 15 katika mgahawa mmoja katibu na mpaka wa Ethiopia, Al Shabaab pia walikiri kuhusika na tukio hilo lililowalenga wanajeshi wa Ethiopia na wangine wa kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM.

Wanamgambo hao walitimuliwa kutoka katika ngome zao kubwa nchini Somalia lakini bado wameendelea kuwa tishio kwa usalama wa nchi hiyo na Afrika Mashariki.

Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC liliidhinisha pendekezo la kuongeza wanajeshi zaidi ili kuzidisha nguvu ya kupambana na wanamgambo hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.