Pata taarifa kuu
DRC

Rais wa DRCongo ateua Tume ya kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Joseph Kabila ameteua Tume maalumu ya kitaifa kwa ajili ya usimamizi na utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyofanyika hivi karibuni. Rais Kabila pia amesaini sheria ya uundwaji wa Tume hiyo itakayoshughulikia masuala kadhaa yanayohitaji utekelezwaji wa dhati.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika uteuzi huo wametajwa pia Maspika wa Bunge la Taifa na lile la Seneti watakaoisimamia Tume hiyo.

Aidha, Rais Kabila amewajumuisha wakuu wa kamati za majadiliano ya kitaifa na watendaji wa ngazi ya chini katika Tume hiyo kwa vile wameziongoza kamati zao katika muda wote wa majadiliano ya kitaifa.

Mwezi uliopita, Rais kabila alihutubia taifa na kuhitimisha mazungumzo ya kitaifa na kutoa ahadi kadhaa kwa ajili ya mshikamano nchini humo ikiwemo uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa itakaojumuisha wadau kutoka pande zote hasa vyama vya upinzani.

Kwa upande mwingine, baadhi ya vyama vya upinzani vyenye msimamo mkali vimetupilia mbali pendekezo hilo la Rais kabila na kubainisha kuwa kilicho cha muhimu ni kuweka misingi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 kwa vile Rais huyo anaelekea mwishoni mwa muhula wake wa pili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.