Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran yaingia katika siku yake ya tatu mjini Ganeva Uswisi

Mazungumzo ya mjini Geneva nchini Uswisi kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran yanaingia katika siku yake ya tatu jumamosi hii wakati wajumbe wa mkutano huo wakijitahidi kuhakikisha wanaafikiana juu ya maswala muhimu kuhusu uwezo wa Tehran katika kurubisha uranium na kutengeneza silaha za nyuklia.

REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ambaye alialikwa kuhudhuria mazungumzo hayo siku ya ijumaa amesema hawajafikia makubaliano kwani bado kuna mambo muhimu ambayo hayajakubaliwa.

Lakini bado kuna matumaini huenda pande hizo zikafikia hatua muhimu licha ya changamoto zinazowakabili katika kufikia muafaka utakaoridhiwa na pande zote.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov anatarajiwa kuwasili mjini Geneva jumamosi hii kushiriki mazungumzo hayo.

Kuwasili kwa Lavrov kutawakutanisha Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yote sita yenye nguvu ambayo kwa takribani muongo mmoja yamekuwa yakizozana na Tehran juu ya mpango huo.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakiishuku Iran kutafuta uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia lakini Tehran imekuwa ikikanusha na kusema kuwa lengo lao ni matumizi salama pakee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.