Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI

Ufaransa kuendeleza uchunguzi juu ya madai ya Al-Qaeda kukiri kuhusika na mauaji ya Wanahabari wawili wa RFI

Licha ya kushindwa kukubali moja kwa moja na madai ya kundi la Al-Qaeda nchini Mali kuhusu kuhusika kwake na mauaji ya waandishi wawili wa habari raia wa Ufaransa mwishoni mwa juma, nchi ya Ufaransa imesisitiza kuendelea na uchunguzi zaidi. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius amesema kuwa wamepokea taarifa kuhusu kuhusika kwa kundi hilo la kigaidi la Al-Qaeda kwenye mauaji ya raia wake wawili waandishi wa habari lakini akasema nchi yake itaendelea kufuatilia madai hayo na kufanya uchunguzi kuwasaka waliohusika.

REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni kundi hilo lilikiri kuhusika na mauaji hayo kwa madai ya kulipiza kisasi kwa Ufaransa ambayo imepeleka wanajeshi wake Kaskazini mwa Mali kukabiliana na makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali ya Bamako.

Katika hatua nyingine, vikosi vya Ufaransa nchini mali vimeendelea na operesheni zake kaskazini mwa taifa hilo kuwakabilia wapiganaji wa makundi ya waasi ambao wanaendelea kutekeleza vitendo vya kihalifu kwenye miji mbalimbali kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa vikosi vya Ufaransa nchini Mali, Kanali Gilles Jaron amekiri kuwa kukabiliana na wapiganaji wa kaskazini mwa Mali ni kazi ngumu kwakuwa wamekuwa na mbinu za kukwepa mashambulizi yao.

Waandishi wa habari wawili wa Ufaransa waliokuwa wakifanya kazi na Radio France International RFI, Ghislaine Dupont mwenye umri wa miaka 57 na Claude Verlont mwenye umri wa miaka 55 waliuawa katika eneo la kilometa chache toka mjini Kidali muda mfupi baada ya kutekwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha mwishoni mwa juma lililopita

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.