Pata taarifa kuu
Nigeria-ICC

Nigeria yahimiza mageuzi kwenye makahama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametetea jana kuhusu mAgeuzi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kama inavyoombwa na Umoja wa Afrika, na kuweka wazi kwamba Nigeria haina mpango wa kujiondowa kwenye mkataba wa Roma.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana kwa mazungumzo jijini Abuja na rais wa mahakama hiyo raia wa Korea Sang Hyun Song, Rais Jonathan amesema hawafikirii kujiondowa kwenye mkataba huo bali wanachofikiria ni kuendelea kushirikiana kwa pamoja kuboresha na kuleta mabadiliko kwenye makahama hiyo.

Ma rais wa nchi kadhaa za Umoja wa Afrika wanaituhumu mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita ya ICC kwa kuwalenga pekee viongozi kutoka katika bara hili tangu pale ilipoanzishwa shughuli zake mwaka 2002.

Octoba 12, viongozi na serikali za Umoja wa Afrika katika kikao kisichokuwa cha kawaida waliomba kuahirishwa kwa kesi inayo mkabili rais wa sasa wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakidai kwamba viongozi waliomadarakani wanaohaki ya kulindwa kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa.

Rais Jonathan amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC inatakiwa kuzingatia changamoto ambazo viongozi wa bara la Afrika wanazokabiliana nazo.

Upande wake rais wa mahakama hiyo, Sang-Hyun Song ametowa wito wa kuendelea kuimarisha mazungumzo ili kutatua matatizo ya Umoja wa Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.