Pata taarifa kuu
Palestina-Mazungumzo

Mamlaka ya Palestina imekataa kuzungumza na Israeli iwapo nchi hiyo itaendelea na ujenzi katika maeneo wanayowania

Utawala wa mamlaka ya Palestina umesisitiza kuwa hauwezi kuendelea na mazungumzo ya amani kati yake na Israeli kuhusu eneo la ukanda wa Gaza iwapo nchi hiyo itaendelea kupanua ujenzi wake wa makazi ya kudumu ya walowezi wa Kiyahudi. Palestina inasema kuwa kamwe hawawezi kujiingiza kwenye mazungumzo yoyote na Israel iwapo nchi hiyo inaendelea na ujenzi wa makazi ya kudumu kwenye eneo ambalo tayari wanaligombea.

Septemba 13 mwaka 1993 waziri mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin na muakilishi wa chama cha OLP, Yasser Arafat.
Septemba 13 mwaka 1993 waziri mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin na muakilishi wa chama cha OLP, Yasser Arafat. REUTERS/Gary Hershorn/Files
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Palestina inatolewa wakati huu ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amewasili mjini Jerusalem na muda mfupi ujao atakuwa na mazungumzo na waziri mkuu Benjamin Netanyahu kujaribu kufufua upya mazungumzo kati ya nchi hiyo mbili.

 Katika hatuwa nyingine, duru sahihi za utawala wa Mamlaka ya wa Palestina, zimearifu kuwa ripoti ya wataalaumu kutoka nchini Uswisi juu ya uchunguzi wa kifo cha kiongozi wa chama cha Fatah Yasser Arafat tayari imewasilishwa.

Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi juu ya kifo cha kiongozi huyo shupavu Taoufiq Tiraoui amesema maabara ya Uswisi iliopewa jukumu la kufanyia uchunguzi kuhusu tuhuma za kupewa sumu kwa kiongozi wa Mamlaka ya wa Palestina na kuwa sababu za kifo chake ipo tayari. Hata hivyo kiongozi huyo hakuongeza lolote hasa kuhusu yaliomo katika ripoti hiyo.

Upande wake maabara hiyo ya Uswisi imejizuia kuzungumza lolote kuhusu ripoti hiyo. Kituo kimoja cha nchini Palestina cha WAFA upande wake kimearifu kuwa wataalamu wa urusi upande wao wamewasilisha ripoti yao tangu Novemba 2 mwaka huu na itawekwa bayana wakati wowote.

Wataalamu zaidi ya sitini walifanya vipimo Novemba 27 mwaka 2012 katika kaburi la Arafatat mjini Ramallah, Cisjordania na kutawanyika katika makundi matatu, Wafaransa, Warusi na wa Swisi.

Arafat alifariki dunia Novemba 11 mwaka 2004 katika Hospitali ya kijeshi jijini Paris nchini Ufaransa ambako alisafirishwa baada ya Israel kutowa kibali kufuatiwa kuwa chini ya ulinzi mkali wa serikali ya Israel.

Sababu za kifo chake hadi leo hazijawekwa bayana, lakini waplaestina wengi wanaamini kwamba Israel ndio waliompa sumu, tuhuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.