Pata taarifa kuu
MISRI

Waziri Kerry azulu Misri kwa mara ya kwanza, aahidi kuunga mkono serikali ya mpito

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amefanya zaiara yake ya kwanza ya kihistoria nchini Misri toka kuangushwa kwa utawala wa rais Mohamed Morsi na jeshi la nchi hiyo ambapo amesisitiza nchi yake kuiunga mkono Serikali ya mpito. 

Waziri wa mambo ya kigeni Marekani John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni Marekani John Kerry RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Kerry mbali na kuunga mkono Serikali ya mpito iliyoko madarakani, ametoa wito kwa viongozi wake kuhakikisha wanatekeleza ahadi yao ya kufanya mabadiliko ya demokrasia nchini humo na kutoa uhuru kwa watu kuandamana.

Waziri Kerry kabla ya kuelekea nchini Saudi-Arabia alikutana na rais wa mpito wa Misri, Adly Mansour pamoja na kiongozi wa jeshi, Abdel Fattah al-Sisi ambao kwa pamoja wamemwahidi waziri Kerry kutoongeza muhula wa wao kubakia madarakani.

Hayo yanajiri huku maelfu ya wafuasi wa Morsi wakiripotiwa kuendelea kukabiliana na polisi kwenye miji mbalimbali nchini Misri wakiwa na mabango yenye picha yake wakishinikiza kuachiliwa huru na kurejeshwa madarakani wakati huu ambapo kiongozi huyo anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo Jumatatu kwa mara ya kwanza tangu kupinduliwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.