Pata taarifa kuu
MISRI

Kesi ya Morsi yaahirishwa hadi Januari 8 mwakani

Rais aliyeondolewa madarakani na jeshi nchini Misri Mohamed Morsi, kwa mara ya kwanza amefikishwa mahakamani hii leo tangu kuondolewa kwake ambapo amepinga uhalali wa yeye kupinduliwa na kutaka viongozi waliofanya hivyo kushtakiwa . 

Rais Mohamed Morsi akiwa katikati ya polisi wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake
Rais Mohamed Morsi akiwa katikati ya polisi wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake firstpost.com
Matangazo ya kibiashara

Morsi na washitakiwa wengine 14 wanatuhumiwa kwa kuchochea vita na mauaji ya waandamanaji nje ya kasri ya ikulu yake mwezi Disemba, madai ambayo huenda yakasababisha kutolewa kwa adhabu ya kunyongwa ama kifungo cha maisha jela.

Morsi ameiambia mahakama kuwa yeye bado ni rais halali wa taifa la Misri na kwamba mahakama hiyo si halali na kuongeza kuwa kilichofanywa na jeshi ni mapinduzi na hivyo viongozi wake lazima washitakiwe.

Huku usalama ukiwa umeimarishwa,Morsi amerudishwa kwenye kambi ya polisi kwa helikopta kabla ya kuwasili kwenye chumba cha mahakama akiwa amevalia suti ya rangi ya blue-nyeusi badala ya mavazi ya watuhumiwa kama ilivyo desturi.

Wafuasi wa Morsi ambao wamejeruhiwa na vurugu pamoja na umwagaji damu uliofanywa na polisi, wanaituhumu serikali iliyowekwa madarakani na jeshi kwa kupika madai dhidi ya Morsi na wameandamana maeneo mbalimbali kwenye mji mkuu kupinga jeshi.

 Aidha kesi yake imeahirishwa hadi mwezi Januari mwaka ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.