Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA

Israel yawaachilia huru wafungwa 26 wa Kipalestina

Israel imewaachia huru wafungwa 26 wa Kipalestina ambao ni kundi la pili kati ya makundi manne yanayotarajiwa kuwa huru ili kufanikisha mchakato wa mazungumzo ya amani kati Israel na Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Wafungwa hao wamepokelewa kwa furaha kubwa na wapendwa wao pamoja na viongozi wa Palestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na kusifiwa kama mashujaa watakaokumbukwa kupigania uhuru wa nchi yao.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas wakati akiwakaribisha wafungwa hao nyumbani amesema kuwa wataendelea kupambana hadi pale wafungwa wote wanaoshikiliwa watakaporudi nyumbani.

Aidha, amesisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote yatakayofikiwa na Israel ikiwa wafungwa wa Kipalestina wataendelea kushikiliwa katika jela za Israel.

Hatua ya kuachiliwa huru kwa wafungwa hao imepongezwa na Marekani kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje John Kerry ambaye amesema kuwa hiyo ni ishara nzuri ya kufanikisha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yaliyovunjika mwaka 2008.

Israel ilikubali kuwaachilia huru wafungwa Wakipalestina 104 kwa awamu nne baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miaka 20 ili kufanikisha kuendelea kwa  mazungumzo hayo ya amani.

Maelfu ya Wapalestina wamekuwa wakishikiliwa katika jela za Israel katika maeneo ya Ukingo za Magharibi, Ukanda wa Gaza na Mashariki mwa Mji wa Jerusalem kuanzia mwaka 1967.

Serikali ya Israel imekuwa ikiwashikilia Wapalestina hao wakiwashtumu kurusha maroketi, mabomu katika ardhi yao na kusababisha mauaji ya Waisraeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.