Pata taarifa kuu
MAREKANI-Mazungumzo

Waziri Mkuu Sharif ataka Marekani kutofanya mashambulizi ya roketi nchini Pakistan

Waziri mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif ameitaka Marekani kuacha matumizi ya ndege za roketi kushambulia nchini Pakistan kwa vile yamekuwa chanzo cha mvutano katika mahusiano ya mataifa.

Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif akiwa ikulu ya Marekani na Raisi Barack Obama 23 October, 2013
Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif akiwa ikulu ya Marekani na Raisi Barack Obama 23 October, 2013 Reuters/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wake na raisi wa Marekani Barack Obama Ikulu ya Marekani jumatano wawili hao waliahidiana kudumisha mahusiano kati ya mataifa yao.

Wakuu hao pia walipata fursa ya kujadili mvutano uliopo baina ya Pakistan na India hususan katika eneo la Kashmir ambalo limekumbwa na hali tete katika siku za hivi karibuni.

Raisi Obama alisema Marekani na Pakistan zitaendelea kuwa washirika muhimu.
Mazungumzo hayo yanakuja muda mfupi baada ya India kuyatuhumu majeshi ya Pakistan kuwafyatulia risasi baadhi ya walinzi wa India wenye jukumu la kulinda mpaka huko Kashmir.

Mlinzi mmoja wa India ameuawa na sita wengine kujeruhiwa kwa mujibu wa vyombo vya habari.

Raisi Obama hakuzungumzia majadiliano yao isipokuwa alimsifia waziri Sharif kwa uamuzi wake wa busara katika kuchunguza kwa namna gani mvutano wenye takribani miongo miwili kati ya India na Pakistan inaweza kushughulikiwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.