Pata taarifa kuu
IRAQ-Mauaji

Mashambulizi yarindima Iraq,28 wauawa wakiwemo polisi 25

Zaidi ya watu 20 wameuawa nchini Iraq baada ya watu wenye silaha na walipuaji wa kujitoa muhanga kushirikiana kutekeleza mashambulizi katika jimbo la Anbar usiku wa kuamkia jumatano.

Zaidi ya watu 20 wameuawa nchini Iraq kufuatia mashambulizi ya kujitoa muhanga
Zaidi ya watu 20 wameuawa nchini Iraq kufuatia mashambulizi ya kujitoa muhanga telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha vifo 28 wakiwemo askari polisi 25 na raia 3 baada ya shambulizi hilo kujiri usiku wa kuamkia jumatano huko magharibi mwa Iraq huku likijeruhi watu 26.

Makundi ya Wanamgambo wakiwemo wale wanaohusihwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda mara kwa mara yamekuwa yakilenga kushambulia majeshi ya usalama ya nchini Iraq na watumishi wa serikali.

Takribani mashambulizi manne yalitekelezwa yakilenga jirani na ndani ya mji wa Rutba penye umbali wa takribani kilomita 110 kutoka eneo lenye rabsha la mpaka wa Syria.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijipua akilenga lori ambalo lilitegeshwa mabomu na kushambulia katika kituo cha polisi mashariki mwa mji, wakati wanamgambo wenye silaha nzito wakishambulia kituo cha polisi cha Rutba na mshambuliaji mwingine akijipua eneo la ukaguzi la polisi huko magharibi.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya polisi na kujeruhi wengien25 wakati raia 3 nao wakipoteza maisha baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanaga kujilipua.

Mnamo mida ya saa 11 usimu kwa saa za Iraq watu wenye silaha walivamia kituo cha polisi huko Ramadi jimbo la Anbar na kuua polisi 3 ,huku 4 wakijeruhiwa.

Mfululizo wa mashambulizi nchini Iraq umeifanya nchi hiyo kuendelea kutishika kiusalama huku lawama zikiendelea kuelekezwa kwa makundi ya kigaidi hususan Al Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.