Pata taarifa kuu
MAREKANI-Ujasusi

Afisa wa Ujasusi Marekani akanusha tuhuma za Kuchunguza mawasiliano ya Ufaransa

Afisa mwandamizi wa ujasusi nchini Marekani James Clapper ametupilia mbali kuwa Washington imekuwa ikichunguza mawasiliano ya simu ya raia wa Ufaransa na kuongeza kuwa hatajadili maelezo zaidi juu ya shughuli zao kwani wanafanya ujasusi kama unaofanywa na mataifa yote kwa maslani yao.

Afisa mwandamizi wa ujasusi nchini Marekani James Clapper
Afisa mwandamizi wa ujasusi nchini Marekani James Clapper Reuters
Matangazo ya kibiashara

Clapper ambaye ni Mkurugenzi wa Ujasusi wa Taifa amesema taarifa za hivi karibuni kuhusiana na upekuzi huo zilizochapishwa na gazeti la Le Monde la nchini Ufaransa hazina uhakika na zinapotosha watu kuhusiana na shughuli za kijasusi za nchi yake.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande alieleza kusikitishwa kwake na taarifa za Marekani kuchunguza kwa siri mazungumzo ya simu ya raia wake, na alizungumza na Rais Barrack Obama kwa njia ya simu na kusema kuwa upekuzi huo haukubaliki huku akitaka maelezo sahihi ni kwanini Marekani inafanya hivyo.

Mapema Jumatatu Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius alitoa agizo kwa Balozi wa Marekani nchini humo kupitia katika Wizara ya Mambo ya nje kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

Naye waziri mkuu wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault ameeleza kushangazwa na kitendo kilichofanywa na Marekani kwa kuona ni makosa kuingilia masuala binafsi ya mawasiliano ya nchi yake pasipo kuwa na sababu za kuridhisha.

Taarifa iliyochapishwa katika gazeti la nchini Ufaransa Le Monde limebainisha kuwa shirika la NSA lilirekodi kwa siri mamilioni ya simu zilizowasiliana ndani ya Ufaransa sambamba na kuingilia anuani pepe ya raisi wa zamani wa Mexico Fellipe Calderon.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.