Pata taarifa kuu
MEXICO-UFARANSA-MAREKANI

Shirika la ujasusi la Marekani laikera Ufaransa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesikitishwa na madai kuwa shirika la kitaifa la Ujasusi la Marekani NASA limemekuwa likichunguza kwa siri mazungumzo ya simu ya raia wake.

Rais wa Ufaransa François Hollande ameeleza kusikitishwa na shirika la ujasusi la Marekani kufanya uchunguzi wa siri dhidi ya mshirika wake.
Rais wa Ufaransa François Hollande ameeleza kusikitishwa na shirika la ujasusi la Marekani kufanya uchunguzi wa siri dhidi ya mshirika wake.
Matangazo ya kibiashara

Holllande amezungumza na rais Barrack Obama kwa njia ya simu na kusema kuwa upekuzi huo haukubaliki huku akitaka maelezo sahihi ni kwanini Marekani inafanya hivyo.

Shirika la NASA limesema limekuwa likisikiliza mawasiliano ya simu nchini Ufaransa na sasa Marekani inasema itabidi iangalie upya mfumo wake wa kufanya uchunguzi wake.

Mapema Jumatatu Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius alitoa agizo kwa Balozi wa Marekani nchini humo kupitia katika Wizara ya Mambo ya nje kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

Naye waziri mkuu wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault ameeleza kushangazwa na kitendo kilichofanywa na Marekani kwa kuona ni makosa kuingilia masuala binafsi ya mawasiliano ya nchi yake pasipo kuwa na sababu za kuridhisha.

Taarifa iliyochapishwa katika gazeti la nchini Ufaransa Le Monde limebainisha kuwa shirika la NSA lilirekodi kwa siri mamilioni ya simu zilizowasiliana ndani ya Ufaransa sambamba na kuingilia anuani pepe ya raisi wa zamani wa Mexico Fellipe Calderon.

Gazeti hilo lilibainisha katika mtandao wake huku likinukuu baadhi ya nakala za Snowden zilizoonesha Shirika hilo la kijasusi lilirekodi takribani simu milioni 70.3 nchini Ufaransa kwa kipindi cha siku 30 kati ya tarehe 10 mwezi desemba na January 8

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.