Pata taarifa kuu
LEBANONI-UTURUKI-SYRIA

Mahujaji wa Lebanoni waliotekwa Syria kwa muda wa miezi 17 wawasili mjini Beirut

Mahujaji 9 raia wa Lebanon waliokuwa wakishikiliwa kama mateka nchini Syria wamewasili mjini Beirut baada ya kuachiwa kuru jana jumamosi, hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano yaliyopelekea pia kuachiwa huru kwa Marubani wawili raia wa Uturuki waliokuwa wakishikiliwa kama mateka nchini Lebanoni.

http://en.tengrinews.kz
Matangazo ya kibiashara

Mahujaji hao toka katika dhehebu la kishia walipokelewa na Baraza la Mawaziri na Maofisa toka serikali ya Lebanon, familia zao nazo zilijumuika kuwalaki wapendwa wao walioonekana kuwa na afya njema ambao wameshikiliwa kama mateka kwa miezi kumi na saba.

Marubani wawili wa Uturuki Murat Akpinar and Murat Agca waliotekwa takribani miezi miwili iliyopita nao waliwasili mjini Istanbul jumamosi usiku na kulakiwa na familia zao pamoja na Waziri Mkuu Recep Teyyip Erdogan.

Marubani hao walishikiliwa na kundi ambalo lilitaka Uturuki itumie ushawishi wake kwa Syria ili iwaachie huru mahujaji 9 wa nchini Lebanon.

Makubaliano ya kuachiwa kwa mateka hayo yaliyohusisha pande tatu, yalikwenda sambamba na wito wa kuachiwa huru kwa wafungwa 200 wa Syria wanaoshikiliwa na utawala wa Rais Bashar al-Assad ingawa bado haijawekwa wazi kama Wasyria hao tayari wamekwishaachiwa huru.

Ndugu wa mahujaji wamekataa kuhusika na kupanga tukio la utekaji wa marubani ambao walitekwa katika eneo linalodhibitiwa na kundi la wapiganaji la Hezbollah, hata hivyo kiongozi mkuu wa kundi hilo Hassan Nasrallah amekanusha kuhusika na tukio hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.