Pata taarifa kuu
MAREKANI

Benki kuu Marekani yaonywa kuhusu msukosuko wa fedha

Viongozi wa taasisi za fedha duniani wametoa wito kwa mamlaka ya benki kuu nchini Marekani kuwa makini wakati wa kupunguza bajeti zao, wakati huu nchi zinazoendelea zikipambana na msukosuko wa fedha. 

Mkutano mkuu wamwaka wa Shirika la fedha duniani IMF
Mkutano mkuu wamwaka wa Shirika la fedha duniani IMF news.xinhuanet.com
Matangazo ya kibiashara

Mataifa Mbalimbali kwenye mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia yamesema kuwa matarajio benki kuu ya Marekani kubanwa tayari ayameongeza changamoto ya uchumi wao, na hivyo kuchochea kuhamishwa kwa kiasi kikubwa cha fedha na kushusha thamani ya fedha yao.

Kamati ya maamuzi ya benki ya dunia, shirika la fedha na kamati ya fedha, zimeionya mamlaka ya benki kuu ya Marekani na benki kuu zingine zenye uchumi mkubwa wanapoanza kurejesha kawaida viwango vyao vya chini vya riba na kurahisisha sera za fedha.

Uchumi wa Marekani na dunia unakabiliwa na viwango vya juu vya riba jambo linaloshusha imani na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi ikiwa bunge la Marekani halitaongeza kiasi cha dola trillion 16.7 za mkopo.

Hazina ya Marekani imesema kwamba itaishiwa fedha za kutosha kulipa madeni yote ya nchi hiyo mapema mwezi Oktoba 17 bila kuongeza madeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.