Pata taarifa kuu
SYRIA

Human Rights Watch yasema waasi nchini Syria waliwaua raia 190

Shirika la Kimataifa la kuteteta haki za binadamu za Human Rights Watch linasema kuwa waasi nchini Syria waliwaua raia 190 na kuwateka wengine 200 wakati wa mapambano na wanajeshi wa serikali mwezi Agosti mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema kuwa mauaji hayo yalitokea katika vijiji ambavyo wafuasi wa rais wa Bashar Al Assad wanaishi wakati wa mapambano hayo.

Katika ripoti hiyo ya kurasa 105 Shirika hilo la haki za Binadamu limesema kuwa limewahoji watu 35 walioponea shambulizi hilo ambalo linawahusisha waasi hao na wanagambo wa Al Qeda.

Kamishena wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Binadamu Navi Pillay amesema kuwa mauaji nchini Syria sasa yanahitaji kushughulikiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC na pande zilizohusika kuchukuliwa hatua.

Kinachoendelea nchini Syria kwa sasa ni hatua ya watalaam wa Umoja wa Mataifa wanaoshughulikia silaha za Kemikali kuharibu viwanda zaidi ya 20 vinavyomilikiwa na serikali ya Syria.

Wataalam hao wanasema kuwa serikali ya Syria inamiliki zaidi ya Tani 1,000 silaha zenye sumu ya Sarin ambazo ni hatari mno na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewataka wataalam hao kuwa makini wanapofanya kazi hiyo kwa kile anachokieleza kuwa ni zoezi ambalo halijawahi kushuhudiwa duniani.

Hatua ya kuharibu silaha hizo za kemikali za Syria lilifikiwa kati ya Marekani na Urusi, na kukubaliwa kuwa zoezi hilo likamilike kufikia tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2014.

Awali, Marekani ilikuwa imetishia kuishambulia Syria kijeshi baada ya kuituhumu serikali ya Assad kutumia silaha hizo za sumu dhidi ya wapinzani wake mjini Damascus na kusababisha mamia ya watu kuuawa mwezi Agosti.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 100,000 wameuawa katika makabiliano kati ya waasi na majeshi ya serikali nchini Syria kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.