Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI

Bunge la Libya laitaka Marekani kumrudisha nyumbani gaidi wa Al Qaeda

Bunge nchini Libya linaitaka Marekani kumrudisha nyumbani mshukiwa wa Al-Qaeda Abu Anas al-Liby aliyekamatwa jijini Tripoli Jumapili iliyopita na Makomandoo wake.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa bunge hilo Omar Hmidan amesisitiza kuwa hatua ya Marekani ilionesha wazi kukiukwa kwa sheria za Kimataifa kwa nchi ya kigeni kuvamia taifa lingine bila ya wenyeji kufahamishwa.

Bunge hilo pia linataka Al-Liby aruhusiwe kuonana na familia yake na kupewa wakili wa kumtetea kwa kile inachosema ni haki ya mshukiwa huyo.

Wanasiasa nchini humo wanasema kuwa nchi yao ina sheria na mshukiwa huyo wa kigaidi anastahili kufunguliwa mashtaka ya kigaidi nchini humo kwa kile wanachosema wana Mahakama ya kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan ametaka Mataifa ya Magharibi kuwasaidia kupambana na Makundi ya Wanamgambo yanyoendelea kujitanua nchini humo huku akisisitiza Marekani inapaswa kumkabidhi Mtuhumiwa wa Ugaidi Abu Anas Al Libi katika nchi hiyo baada ya kumkamata.

Kauli ya Waziri Mkuu wa Libya Zeidan imeendelea kujibiwa na Marekani kupitia Rais wake Barack Obama ambaye ameithibitishia dunia wao wana ushahidi wa kutosha unaonesha Al Libi alihusika kwenye mashambulizi ya kigaidi na atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mapema juma hili Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry pia alikanusha madai ya Libya kuwa mshukiwa huyo alitekwa nyara na Serikali ya Libya haikushauriwa wakati wa kukamatwa kwa mshukiwa huyo.

Abu Anas al-Liby anatuhumiwa na Marekani kuongoza mashambulizi ya kigaid katika Ubalozi wake nchini Kenya na Tanznaia mwaka 1998 na kusababisha zaidi ya watu mia mbili kuuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.