Pata taarifa kuu
KOREA-MAREKANI

Manuari ya kivita ya Marekani yawasili Pwani ya Korea Kusini

Serikali ya Korea Kaskazini imewataka wanajeshi wake kuwa tayari kupambana baada ya kuwasili kwa manuari ya kivita ya  Marekani kupanga kuongoza mazoezi ya kijeshi  ikishiriakiana na Korea Kusini na Japan.

Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya Seoul na Washington DC kutia saini makubaliano ya kuweka mikakati ya kufanya mazoezi ya pamoja kujiweka tayari kupambana na Pyongyang ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikiendelea na mazoezi ya kijeshi na kujaribu silaha zake za Nyuklia.

Wachambuzi wa siasa za Korea wanasema kuwa maandalizi ya mazoezi haya ya Marekani na washirika wake pamoja na vitisho vya Korea Kusini yanahatarisha kutofanyika kwa mazungumzo ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo kuhusu silaha hizo za Nyuklia.

Jeshi la Marekani lilikuwa limetangaza kuanza  mazoezi hayo Pwani ya Korea Kusini  siku ya Jumanne lakini imeahirisha kutokana na bahari kuchafuka.

Korea Kaskazini imekashifu maandalizi ya mazoezi hayo kwa kile inachosema Marekani na washirika wake wanaanda vita dhidi yao.

Jeshi la Korea Kaskazini limeitaka Marekani kufahamu kuwa jeshi lake liko tayari kupambana nao ikiwa litaingilia mambo yake.

Msemaji wa jeshi la Korea Kusini Kim Min Seok amesema kuwa jeshi lake linachunguza mwenendo wa jeshi la Korea Kaskazini ambalo limeendelea kuonesha nia ya kuivamia.

Marekani imekuwa ikisema kuwa itaendelea kutetea washirika wake kutokana na vitisho vya Korea Kaskazini ambavyo vimekuwa ni vya kuivamia Korea Kusini.

Uhusino kati ya nchi hizi mbili ulidhoofika zaidi baada ya Korea Kaskazini kuizamisha meli ya Korea Kusini mwaka 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.