Pata taarifa kuu
IRAQ

Ghasia Iraq 51 wafariki zaidi ya 100 wajeruhiwa

Takribani watu 51 wameuawa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililolenga washia huko mji mkuu wa Iraq Baghdad,wizara ya mambo ya ndani imethibitisha.

Moja kati ya shambulizi la hivi karibuni mjini Baghdad nchini Iraq
Moja kati ya shambulizi la hivi karibuni mjini Baghdad nchini Iraq REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Balad shambulizi la kujitoa muhanga limeua takribani watu 12 katika mgahawa wakati na huko Masul watu wenye silaha wameshambulia na kuua waandishi wa habari wawili.

Iraq imeendelea kushuhudia vita vya kidini katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni matukio ambayo yameyumbisha hali ya usalama nchini humo.

Hata hivyo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulizi hilo la jumamosi ingawa matukio mengi ya hivi karibuni yamekuwa yakitekelezwa na mashirika ya kisuni yenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeada.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.