Pata taarifa kuu
MISRI

Watu wanne wauawa katika ghasia zilizozuka baada ya swala ya ijumaa jijini Cairo

Makabiliano yaliyozuka jana ijumaa nchini Misri baina ya polisi na wafuasi wa kiongozi aliyeondolewa madarakani na jeshi Mohamed Morsi yamesababisha vifo vya watu wanne mjini Cairo. Ghasia hizo zilizozuka baada ya swala ya ijumaa zilishudiwa pia katika miji ya Alexandria na Assiut na inadaiwa watu zaidi ya 45 walijeruhiwa.

REUTERS/ONTV Live via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Akithibitisha idadi ya vifo na majeruhi, Mkuu wa kitengo cha huduma za dharura nchini humo Khaled al-Khatib amesema hakuna polisi wala mwanausalama yeyote aliyeuawa katika machafuko hayo.

Polisi walimimina risasi hewani na kurusha mabomu ya machozi kuwakabili waandamanaji karibu na bustani ya Tahrir ambayo ni kitovu cha kuanza kwa mabadiliko ya Taifa hilo.

Wanachama wa Muslim Brotherhood zaidi ya 2000 wanashikiliwa na vyombo vya usalama tangu kuanza kwa machafuko hayo mwezi Julai mwaka huu.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Kiongozi wa juu wa chama hicho Generali Mohammed Badie anayetuhumiwa kuchochea ghasia na mauaji.

Bado haijafamika ni lini Morsi atatolewa katika eneo la siri analoshikiliwa toka alipoondolewa madarakani na tayari chama chake kimepigwa marufuku ya kuendesha shughuli zake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.