Pata taarifa kuu
ITALIA

Juhudi za kutafuta miili ya wahamiaji haramu toka Afrika waliopata ajali ya boti zinatarajiwa kuendelea tena jumamosi hii

Juhudi za kutatufa mamia ya miili ya wahamiaji haramu toka barani Afrika waliopoteza maisha katika ajali ya boti kwenye bahari ya Mediterranean zinatarajiwa kuendelea tena hii leo baada ya kufanikiwa kupata maiti 111 katika siku ya kwanza ya zoezi hilo. Zoezi hilo lilisitishwa kwa muda kutokana na hali mbaya ya hewa na vikosi vya uokoaji vinasema huenda miili mingine imepelekwa mbali zaidi kutokana na mawimbi makubwa kupiga baharini.

REUTERS/Antonio Parrinello
Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo inayokadiriwa kuwa na wahamiaji takribani mia sita wengi wao kutoka mataifa ya Eritrea na Somalia iliungua na kisha kuzama karibu na visiwa vya Lampedusa.

Serikali ya Italia imetoa wito kwa nchi nyingine za bara la Ulaya kuweka sheria kali zaidi ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia huko kwa njia zisizo rasmi.

Umoja wa Mataifa UN umesikitishwa na tukio hilo na kusema umefika wakati wa kuhakikisha harakati za wahamiaji haramu zinadhibitiwa ili kuepusha majanga yanayoendelea kushuhudiwa.

Naye kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis alisema ni vyema wahamiaji hao wakawa na utaratibu wa kufikiria kwanza athari za kutumia njia haramu kabla ya kufikia uamuzi wa kuelekea barani Ulaya.

Wahamiaji zaidi ya 30,000 wameripotiwa kuingia nchini Italia mwaka huu, idadi ambayo ni mara nne ya walioingia mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.