Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Mahakama Kuu Nchini Bangladesh yamhukumu adhabu ya kifo Mbunge Chowdhury baada ya kumkuta na hatia ya Mauaji

Mahakama Kuu nchini Bangladesh imemhukumu adhabu ya kifo Mbunge wa Kwanza na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Upinzani Cha Bangladesh Nationalist BNP Salauddin Quader Chowdhury baada ya kumkuta na hatua ya kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1971.

Mbunge wa Bangladesh na Kiongozi wa Upinzani Salauddin Quader Chowdhury amehukumiwa adhabu ya kifo
Mbunge wa Bangladesh na Kiongozi wa Upinzani Salauddin Quader Chowdhury amehukumiwa adhabu ya kifo
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu ya Bangladesh imemkuta na hatua Chowdhury ya kutenda makosa ya uhalifu wa kivita ikiwemo mauaji na kufanya mateso kwa wananchi kwa mgongo wa dini wakati wa vita vilivyotokea mwaka 1971 baada ya nchi hiyo kujipatia uhuru wake.

Hukumu hiyo imerejesha hali ya wasiwasi na kumekuwa na hofu huenda kukatoke machafuko kwa mara nyingine baada ya hapo awali kushuhudia hali kama hiyo baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Jamaat-e-Islam kuhukumiwa adhabu ya kifo.

Chowdhury mwenye umri wa miaka 64 anatakiwa anyongwe hadi kufa ikiwa ni sehemu ya kutekelezwa kwa adhabu aliyopewa Kiongozi wa Jopo la majaji lililokuwa linaskiliza kesi yake A.T.M Fazle Kabir amewaambia mamia ya watu waliojitokeza mahakamani hapo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mahbubey Alam amewaambia wanahabari wamefurahishwa mno na hukumu iliyotolewa na Mahakama dhidi ya Chowdhury wakisema inaweza ikawa funzo kwa watu wengine ambao wamekuwa na mtazamo kama wake.

Upande wa utetezi wenyewe umepingana na hukumu iliyotolewa wakidai imekuja kutokana na shinikizo kutoka kwa Serikali na ilishaandaliwa na Wizara ya Sheria na kukabidhiwa Majaji hao kwa ajili ya kuisoma tu.

Mwanasheria wa Chowdhury, Fakhrul Islam amesema lengo la kuhumu hiyo ni kutaka kunyamazisha sauti ya Upinzani ambao umekuwa ukimpa wakati mgumu Waziri Mkuu Sheikh Hasina.

Wafuasi wa Chama Cha BNP alichokuwa anakiongoza Chowdhury kimejiapiza kujitokeza mitaani kupinga kwa nguvu zao zote hukumu iliyotolewa wakidai haijafuata taratibu zinazofaa na badala yake shinikizo limekuwa kubwa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Chandan Kumar Chakrabarty amesema wameshasambaza askari wa kutosha kwenye mitaa yote katika kuhakikishwa wanakabiliana na maandamano yanayotarajiwa kufanywa na wafuasi wa Chowdhury.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.