Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Pakistani wafanya jitihada kunusuru maisha yao

Waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Pakistani lililosababisha vifo vya takribani watu 348, wanafanya jitihada za kujiokoa huku mabaki ya miamba na udongo vikikwamisha jitihada hizo.

Waathirika wa tetemeko la ardhi wakifanya jitihada kujinusuru
Waathirika wa tetemeko la ardhi wakifanya jitihada kujinusuru washingtonpost.com
Matangazo ya kibiashara

Manusura Kusini Magharibi mwa Pakistan wanalazimika kulala kwa kupeana zamu katika malazi yaliyojengwa kwa miti na shuka baada ya nyumba zao za tope kusawazishwa katika tetemeko hilo kubwa la ardhi ambalo limeua mamia.

Mamlaka ya taiafa ya majanga nchini humo imesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia siku ya Jumanne ni 348 lakini vyanzo vingine vimeeleza kuwa idadi ya vifo imefikia watu 500.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcher 7.7 lilipiga katika wilaya ya Awaran katika jimbo la Balochistan na kuwaacha wakaazi maelfu wa eneo hilo wakiwa hawana makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.