Pata taarifa kuu
MISRI-MAANDAMANO

Umwagaji wa damu waendelea kushuhudiwa nchini Misri ambapo polisi imewashambulia waandamanaji Muskitini

Wafuasi wa kiongozi aliepinduliwa madarakani wa chama cha Muslim Bradherhood nchini Misri, wameendelea kutowa wito wa kuandamana kuwashinikiza viongozi wa kijeshi kuurejesha utawala uliokuwepo na kuacha kuwatia nguvuni waandamani wanaendelea kuandamana katika miji mbalimbali nchini humo.

Msikiti wa  al-Fath uliozingirwa na polisi tangu Agosti 16
Msikiti wa al-Fath uliozingirwa na polisi tangu Agosti 16 REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Habari za hivi punde zaarifu kuwa polisi wanaozingira Muskiti mmoja walikokusanyika wafuasi wa kiongozi huyo wa Misri Mohamed Morsi, wamewafiatulia risase watu waliokuwa muskitini baada ya kudai kuwa walishambuliw ana watu waliokuw andani ya muskiti huo.

Hayo yanakuja siku moja baada ya kutokea vifo vya watu zaidi ya thmanini waliouawa jana wakati wa maandamano makumbwa ya baada ya sala ya Ijumaa.

Machafuko yanatoendelea nchini Misri yanaendelea kuamsha hisia mbalimbali ulimwenguni ambapo jana ma mia ya waislam katika miji ya Kharthoum nchini Sudan, Amman, Rabat, Jerusalem mashariki na Scijordania wameandamana kuonyesha uungwaji mkono wa kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliofanywa na jenerali Abdel Fattah al-Sissi.

Wakati huo huo viongozi wa ulaya wamendelea kukutana ili kutowa ujumbe mzito kuhusu hali inayoendelea nchini Misri, huku waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani akikutana na mwenziwe wa Qatar Khaled Al Attiya kuzungumzia kuhusu hali inayoendelea nchini Misri na Syria.

Katika mji wa Nazareth nchini Israel Makundi ya kiislam ya kiarabu yametowa wito wa kuandamana leo kuonyesha uungwaji mkono kwa ndugu zao wa huko Misri na kuendelea kuwaombe waislam walipoteza maisha siku ya Jumatano baada ya kushambuliwa na vikosi vya usalama.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.