Pata taarifa kuu
IRAQ

Milipuko ya mabomu yaua watu zaidi ya sitini mjini Baghdad

Watu zaidi ya sitini wameuawa na wengine zaidi ya mia mbili kujeruhiwa katika mfululizo wa milipuko ya mabomu ya kutegwa kwenye magari katika mji mkuu wa Iraq Baghdad, mashambulizi hayo yametekelezwa wakati waumini wa dini ya kiislamu wakiendelea kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr.

REUTERS/Thaier al-Sudani
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mashambulizi nchini humo ambapo watu zaidi ya mia nane wameripotiwa kuuawa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani pekee.
 

Takwimu zaidi juu ya mauaji ya nchini humo zinasema kuwa watu zaidi ya elfu tatu wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Vikosi vya usalama vimekuwa katika jitihada za kupambana na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Qaeda linalotajwa kuratibu mashambulizi kadhaa dhidi ya vikosi vya serikali, vikosi vya kigeni na raia.

Hivi karibuni Marekani ilitangaza donge nono la dola milioni kumi kwa yoyote atakayefanikisha kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Abu Bakr a-Baghdadi ambaye inaaminiwa yuko nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.