Pata taarifa kuu
MISRI

Wafuasi wa rais Morsi wapambana na polisi jijini Cairo

Wafuasi wa raisi aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohamed Morsi jana Ijumaa wamefanya mikutano ya hadhara na kupambana na polisi jijiji Cairo, baada ya serikali kuamuru kuvunjwa kwa kambi zao za maandamano 

Wafuasi wa Morsi wakipambana na polisi jijini Cairo
Wafuasi wa Morsi wakipambana na polisi jijini Cairo english.ruvr.ru
Matangazo ya kibiashara

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji takribani 1,000 ambao walijaribu kuweka kambi mpya nje ya eneo kubwa la vyombo vya habari.

Mapigano hayo yalianza baada ya mjumbe wa Marekani William Burns kuwasili jijini Cairo, hii ikiwa ni ziara ya karibuni ya mjumbe wa kimataifa yenye dhamira ya kuwashawishi wafuasi wa Morsi na serikali ya mpito kutatua msuguano uliopo kwa amani.

Wakati huo huo, Ayman al-Zawahiri, kiongozi wa wapiganaji wa Al-Qaeda na mzaliwa wa Misri ameishutumu Marekani kwa kupanga njama za kuangushwa kwa rais Morsi kwa kushirikiana na kijeshi pamoja na wakristo wachache.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.