Pata taarifa kuu
MALI

Ibrahim Boubacar Keita aendelea kuongoza katika matokeo ya awali Urais wa Mali

Waziri Mkuu wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keita anaongoza katika matokeo ya awali ya kura za Urais zilizopigwa na wananchi wa Taifa hilo mwishoni mwa juma lililopita. Keita mwenye umri wa miaka 69 anaongoza hivi sasa akifuatiwa na Soumaila Cisse ambaye amewahi kuwa Waziri wa Fedha.

AFP PHOTO GEORGES GOBET
Matangazo ya kibiashara

Mchuano mkali umeendelea kusalia kati ya wagombea wawili pekee miongoni mwa 27 walioshiriki kinyang'anyiro hicho.

Kiongozi wa waangalizi wa uchaguzi huo toka Umoja wa Ulaya EU wametoa wito kwa wananchi kuheshimi matokeo ya kura zao ambayo huenda yakatangazwa siku ya ijumaa.

Mataifa mbalimbali yamewasifu amani na utulivu iliyoonyeshwa na wananchi wa Taifa hilo waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na kutupilia mbali vitisho vilivyotolewa na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa MUJAO kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwenyekiti wa jumuia ya Nchi za Afrika magharibi ECOWAS akiwa pia raisi wa Cote D'Ivoire Alassane Ouattara amesema kuwa ameridhika na namna ambavyo wananchi wameshiriki zoezi hilo kwa kusema hatua hiyo ni njia halisi ya kufikia amani wanayoitafuta.

Naye Raisi wa Burkina Faso, Blaise Compaore amesema raisi mpya wa Nchi hiyo ya Mali atakuwa na jukumu kubwa la kurejesha amani na umoja wa kitaifa nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi huo yanayoendelea kusubiriwa kwa hamu kubwa yatamaliza uongozi wa serikali ya mpito iliyoingia madarakani baada ya kufanyika mapinduzi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa nchini hiyo Amadou Touman Toure.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.