Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Mamnoon Hussain atangazwa kuwa Rais mpya wa Pakistan

Mfanyabiashara maarufu Mamnoon Hussain toka chama cha PML-N nchini Pakistan amechaguliwa kuwa Rais wa 12 wa Taifa hilo, Hussain anakuwa mrithi wa Asif Ali Zardari ambaye muhula wake wa miaka mitano ya Urais wa Taifa hilo unamalizika mwezi septemba mwaka huu.

AFP PHOTO /AAMIR QURESHI
Matangazo ya kibiashara

Hussain amejipatia kura 432 wakati mpinzani wake wa karibu Wajihuddin Ahmed akipata kura 77, Mkuu wa tume ya uchaguzi Fakhruddin Ebrahim amethibitisha matokeo hayo.

Wakati Rais mpya wa nchi hiyo akitangazwa wanausalama wanaendelea na msako mkali mara baada ya Wanamgambo wa Taliban kutekeleza shambulizi kwenye gereza moja katika mji wa Dera Ismail Khan kaskazini magharibi mwa Pakistani ambapo Wafungwa takribani 250 walifanikiwa kutoroka.

Watu wapatao 12 wakiwemo askari wanne waliuawa na saba wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililotekelezwa na wanamgambo waliokuwa wamevalia sare za polisi ambao walikabiliana vikali na vikosi vya Usalama, Maafisa nchini Pakistani wamethibitisha.

Wafungwa sita kati ya waliotoroka walikamatwa na polisi, 30 miongoni mwa waliofanikiwa kutoroka ni wanamgambo.

Polisi na vikosi vingine vya dharura wanafanya msako na kutangaza hali ya hatari huku wakiwataka Raia kubaki majumbani mwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.