Pata taarifa kuu
MISRI

Wafuasi wa Morsi waendelea na maandamano ya kushinikiza kuachiwa Kiongozi wao huku idadi ya waliouawa ikifikia 13

Maandamano makubwa yameendelea kufanyika nchini Misri yakiwa na lengo la kumshinikiza Kiongozi wa Mpito Adly Mahmud Mansour kumuachia Mohamed Morsi ambaye anashikiliwa na Jeshi tangu alipoondolewa madarakani na kipindi hiki idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia watu 13.

Wafuasi wa Mohamed Morsi wakikabiliana na wale wanaoiunga mkono Serikali ya Adly Mansour na kusababisha vifo vya raia
Wafuasi wa Mohamed Morsi wakikabiliana na wale wanaoiunga mkono Serikali ya Adly Mansour na kusababisha vifo vya raia REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Morsi wamekuwa mstari wa mbele kukabiliana na Jeshi la Polisi ambalo limekuwa mstari wa mbele kuzima maandamano hayo yanayozidi kuchukua sura mpya kila uchao kitu ambacho kinaongeza hofu ya usalama kwa wananchi na wengi wakihisi kutakuwa na mgawanyiko.

Maandamano hayo yalizuka siku ya jumatatu na kuendelea siku ya jumanne na kuchangia mamia ya wafuasi wa Morsi kujeruhiwa kutokana na Jeshi la Serikali kukaa imara kuzima ghasia ambazo zimeendelea kufanyika katika Jiji la Nasr na hata Cairo.

Wafuasi wa Morsi waliamua kuanzisha maandamano upya kutokana na familia yake kujitokeza na kuweka bayana dhamira yake ya kutaka kumshtaki Mkuu wa Majeshi nchini humo Jenerali Abdel Fattah Al Sisi kutokana na kumshikilia Kiongozi huyo wa zamani.

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Misri imeshatoa onyo kali kwa wale wote ambao watakuwa mstari wa mbele kuvunja sheria kwa kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku na wametoa wito wa kuimarishwa kwa amani.

Ghasia ambazo zinaendelea nchini Misri zimeendelea kugharimu uhai wa raia kwani takwimu zinaonesha katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita idadi ya watu kumi na watatu wamepoteza maisha huku magari kumi na sita yakichomwa moto.

Polisi wanane waliokuwa kwenye harakati za kukabiliana na maandamano hayo wamejeruhiwa kutokana na wafuasi wa Morsi kurusha maguruneti kulenga kituo cha Polisi katika eneo la Dahqaliya.

Utawala wa Misri umeendelea kusisitiza Morsi yupo sehemu salama kabisa na wanamshikilia kwa muda wote huu kwa sababu za usalama na pindi wakatapojiridhisha hali imetengamaa basi watamuachia.

Wanachama wa Chama Cha Muslim Brotherhood wamejiapiza kuendelea na maandamano yao hadi pale ambapo Morsi ataachia na kusha akabidhiwe madaraka yake kwa kuwa alichaguliwa kwa njia za kidemokrasia lakini ameondosha mamlakani kwa kutumia Jeshi.

Tayari Mkuu wa Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameshaitaka Serikali ya Cairo kutoa maelezo juu ya kuendelea kushikiliwa kwa Morsi huku wakitaka Kiongozi huyo aachiwe mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.