Pata taarifa kuu
LEBANON-UBELGIJI-ULAYA

Umoja wa Ulaya EU walijumuisha Kundi la Hezbollah kwenye orodha ya Makundi ya Kigaidi Duniani

Umoja wa Ulaya EU kupitia Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wamekubaliana kuliweka kwenye orodha ya Makundi ya Kigaidi Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah la nchini Lebanon.

Nembo inayotumika kutambulisha Umoja wa Ulaya EU iliyopo katika Makao Makuu yake huko Brussels nchini Ubelgiji
Nembo inayotumika kutambulisha Umoja wa Ulaya EU iliyopo katika Makao Makuu yake huko Brussels nchini Ubelgiji
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya Nje wamekubaliana kuliweka Kundi hilo kwenye orodha hiyo ya Makundi ya Kigaidi Duniani kitu ambacho kitamuweka matatani mtu yoyote ambaye atakuwa tayari kulifadhili kundi hilo.

Kundi la Hezbollah ambalo kwa sasa limekuwa likiisaidia serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al Assad kwenye vita dhidi ya Waasi limekuwa likitajwa kuwa ni hatari kwa usalama na ndiyo maana limewekwa kwenye orodha hiyo.

Hatua ya Umoja wa Ulaya EU kuliweka Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi imekuja kutokana na kushinikizwa kwa muda mrefu kufanya hivyo na Marekani pamoja na washirika wao Israel.

Kundi la Hezbollah kwa sasa limeingia kwenye orodha ya makundi mengine yakiwemo Taliban, Al Qaeda na Al Shabab ambayo nayo yametajwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi kutokana na matukio wanayoyafanya.

Israel imekuwa ni miongoni mwa mataifa ya kwanza kupongeza hatua ya Umoja wa Ulaya EU kuliorodhesha Kundi la Hezbollah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na hivyo kuanzia sasa litakuwa linapigwa vita.

Waziri wa Sheria wa Israel Tzipi Livni amekiri wamepokea kwa furaha uamuzi huo kwa sababu Kundi la Hezbollah limekuwa likifanya vitendo vya kigaidi na hivyo walipaswa kuwepo kwenye orodha hiyo muda mrefu uliopita.

Taifa la Uholanzi nalo halikuwa nyuma kupongeza kile ambacho kimefikiwa na Umoja wa Ulaya EU kupitia Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchini 28 kwa kusema uamuzi huo ulikuwa muafaka dhidi ya Kundi la Hezbollah.

Waziri wa Mambo ya Nje Frans Timmermans amesema hakukuwa na sababu ya kuacha kuliweka Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah kwenye orodha hiyo ya makundi ya kigaidi kutokana na vitendo ambavyo wamekuwa wakivifanya.

Kundi la Hezbollah limekuwa likipingana na Serikali ya Israel kwa muda mrefu kitu ambacho kimechangia kwa kiasi kikubwa kuwa maadui na hivyo kushinikiza kutambulika kwa Kundi hilo kama moja ya Makundi ya Kigaidi kitu ambacho wamefanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.