Pata taarifa kuu
MISRI-MAANDAMANO-MAREKANI

Mashaka yaibuka juu ya uteuzi wa Elbaradei kushika wadhifa wa Uwaziri mkuu Misri

Msemaji wa kiongozi wa mpito nchini Misri Adly Mansour amearifu kuwa mchakato bado unafanyika ili kumpata waziri mkuu wa taifa hilo wakati huu ambapo kumekuwa na tetesi za kuteuliwa Mohamed Elbaradei ambaye amekosolewa kutofaa kushika wadhifa huo.

Maandamano yameripotiwa nchini Misri kwa pande zinazompinga na kumuunga mkono Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani na jeshi hivi karibuni.
Maandamano yameripotiwa nchini Misri kwa pande zinazompinga na kumuunga mkono Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani na jeshi hivi karibuni. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za kiofisi zilimtaja kushika wadhifa huo bwana ElBaradei ambaye ni kiongozi wa zamani muangalizi wa masuala ya nyuklia katika umoja wa mataifa UN.

Taarifa za kuteuliwa kwake zimekuwa zikikosolewa kwa madai kuwa kiongozi huyo asingefaa kwa chochote.

Wakati katibu wa umoja wa mataifa UN Ban Ki Moon akiwataka viongozi kuhakikisha waandamanji wanalindwa na kuwa salama serikali ya Marekani imewataka viongozi wa Misri kukomesha ghasia.

Tayari Mataifa makubwa duniani yameonesha kuguswa na hali ya mambo nchini Misri ambapo sasa hali ya Utulivu imeendelea kupotea nchini humo kufuatia usiku wa mapigano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.