Pata taarifa kuu
MISRI-MORSI

Rais Mohamed Morsi wa Misri apinduliwa na jeshi, historia ya Hosni Mubarak yajirudia

Jeshi nchini Misri limempindua na kumkamata Rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi hapo jana baada ya vurugu za juma zima na maandamano yaliyokuwa yakishinikiza Rais huyo kujiuzulu.Mapinduzi hayo yanafanyika ikiwa ni mwaka mmoja tangu aingie madarakani baada ya kung'olewa madarakani kwa Rais wa zamani Hosni Mubarak kwa kilichodaiwa alikiuka misingi ya demokrasia.

REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo ya Misri Jenerali Abdel Fattah al-Sisi alitangaza kwa njia ya Televisheni taarifa za kuangushwa kwa Rais Morsi.

Kufuatia mapinduzi hayo Jaji Mkuu Adly al-Mansour ataongoza serikali ya mpito kabla kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia utakaofanyika baadaye nchini humo.

Kulingana na mpango wa jeshi jaji huyo mkuu anaapishwa leo Alhamisi na kuchukua nafasi ya kuongoza serikali ya mpito itakayoundwa.

Polisi nao waliwazingira wasaidizi wa Morsi na Viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood, huku hati za kuwakamata wafuasi 300 wa Chama hicho zikitolewa.

Morsi na Wasaidizi wake wa juu wako kizuizini katika eneo la kikosi cha ulinzi wa Rais wa Misri hali ambayo imezua hasira kwa wafuasi Chama cha Muslim Brotherhood .

Juma lililopita takriban watu 50 waliuawa baada ya kuwepo mapigano baina ya Wafuasi wa Chama cha Muslim Brotherhood na Upinzani.

Awali Ofisi ya Rais nchini Misri ilikataa kutekeleza matakwa ya Jeshi na kusema kuwa itaendelea na mipango yake ya kulipatanisha taifa hilo.

Jeshi nchini Misri lilimuasa Rais Mohamed Morsi kuwa litaingilia kati ikiwa atashindwa kutekeleza matakwa ya Raia ndani ya saa 48.

Taarifa ya Ofisi ya Rais ilikemea hatua ya jeshi kutaka kuingilia kati na kudai kuwa hatua ya jeshi hilo italeta mgawanyiko zaidi na kutishia kuvunjika kwa amani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.