Pata taarifa kuu
MISRI-MORSI

Jaji Mkuu Adly al-Mansour aapishwa kuongoza serikali ya mpito Misri baada ya mapinduzi

Jaji Mkuu Adly al-Mansour ataongoza serikali ya mpito kabla kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia utakaofanyika baadaye nchini humo Kufuatia mapinduzi yalifanyika nchini Misri.Jaji Mkuu Adly al-Mansour Kulingana na mpango wa jeshi jaji huyo mkuu ameapishwa leo Alhamisi na kuchukua nafasi ya kuongoza serikali ya mpito itakayoundwa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kupishwa kwa jaji imekuja baada ya Jeshi nchini Misri kumpindua na kumkamata Rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi jana kufuatia vurugu za juma zima na maandamano yaliyokuwa yakishinikiza Rais huyo kujiuzulu.

Akiapishwa mahakama ya juu ya katiba, Adly al-Mansour ameahidi katiba na utawala wa sheria na ataongoza serikali ya mpito kwa kulinda matakwa na vipaumbele vya raia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema kuwa hatua ya jeshi la Misri kuingilia kati na kuuondoa utawala uliowekwa madarakani kwa njia za kidiplomasia si sahihi.

Amema kuwa kitendo hicho kinarudisha nyuma jitihada za kukuza demokrasia nchini humo na ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na kufikiwa kwa muafaka wa kisiasa kwa ajili ya mustakabali wa baadaye wa Misri.

Guido Westerwelle amebainisha kuwa mapinduzi hayo ni hatari kwa nchini ya Misri na kipindi cha mpito kuelekea demokrasia ya kweli kimevurugwa na kuharibiwa vibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.