Pata taarifa kuu
MISRI-MORSI

Rais wa Misri Mohamed Morsi aonya juu ya mgawanyiko wa kisiasa nchini humo

Rais wa Misri Mohamed Morsi ametoa onyo kali kwa wananchi wa Taifa hilo kuacha kugawanywa kwa misingi ya kisiasa kwani hatua hiyo inaweza ikalemaza shughuli za kiuchumi tamko linalokuja kipindi hiki wafuasi wake na wakosoaji wake wakipambana na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Rais wa Misri Mohamed Morsi
Rais wa Misri Mohamed Morsi
Matangazo ya kibiashara

Tamko la Rais Morsi amelitoa wakati akihutubia taifa alipotimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani kupitia uchaguzi mkuu, huku akitumia fursa hiyo pia kubainisha mafanikio yaliyopatikana kwa muda huo na kulitaka jeshi kuacha kuingilia masuala ya kisiasa.

Wachambuzi wa Siasa wanaonakuwa tatizo kubwa linalochangia mambo yaendelee kuchafuka nchini Misri ni kutokana na katiba iliyopo kama anavyoeleza Mchambuzi wa Siasa kutoka kenya Balozi Bethwell Kiplagati.

wakati kiongozi wa taifa hilo akiadhimisha sherehe za mwaka mmoja tangu pale alipochukuwa hatamu ya kuiongoza nchi hiyo, Upinzani umetowa wito wa maandamano kumshnikiza rais Morsi kujiuzulu, kufuati kile wanachodai ameshindwa kutatuwa matatizo yanayo wakumba wananchi wa taifa hilo.

wafuasi wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono kiongozi huyo kutoka mrengo wa chama cha Muslim Bradherhood juma lililopita wameandamana kumuunga mkono rais Morsi wakidaikuwa rais aliye chaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia hawezi kuenguliwa kupitia maandamano.

Kumekuwa na harakati nchini humo za kukusanya sahihi zitazo wezesha kutishwa kwa uchaguzi kabla ya wakati, jambo ambalo laonakana kutokwa rahisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.