Pata taarifa kuu
Ufaransa-Syria

Raisi wa Ufaransa awasili Qatar katika juhudi za kuwawezesha waasi wa syria

Raisi wa Ufaransa Francois Hollande amewasili nchini Qatar tayari kwa mazungumzo juu ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Syria na kujadili mahusiano ya kiuchumi na taifa hilo lenye utajiri wa gesi.

Raisi wa Ufaransa Francois Hollande awasili Qatar katika juhudi za kuwezesha upinzani wa Syria kupambana dhidi ya majeshi ya serikali.
Raisi wa Ufaransa Francois Hollande awasili Qatar katika juhudi za kuwezesha upinzani wa Syria kupambana dhidi ya majeshi ya serikali. REUTERS/Andrew Winning
Matangazo ya kibiashara

Raisi Hollande amejumuika nchini humo kufuatia mkutano wa mataifa rafiki za Syria katika siku iliyoamuliwa kutolewa haraka kwa msaada wa kijeshi kuwasaidia waasi wa Syria.
Aidha raisi Hollande alizungumza katika mkutano wake na wafaransa waishio Qatar na kusema kuwa amekaribisha maamuzi ambayo yataruhusu kuunga mkono upinzani nchini Syria ili kufikiwa lengo la kupatikana suluhu ya kisiasa.

Mawaziri kutoka uingereza, misri, ufaransa, Ujerumani, Italia, Jordan, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki na marekani kwa pamoja walihudhuria mazungumzo hayo.

Tamko la mwisho lilikuwa ni kwa kila nchi kwa namna yake ingetoa haraka mahitaji na vifaa vyote muhimu ili kuwawezesha waasi kuwalinda watu wa Syria pia kukabiliana na mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na majeshi ya serikali na washirika wake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.