Pata taarifa kuu
SYRIA-AUSTRIA-ISRAELI

Serikali ya Austria yataka Wanajeshi wake wanaolinda Amani katika Eneo la Golan kuondoka baada ya wanajeshi wawili kujeruhiwa

Serikali ya Austria imetangaza kuondoa wanajeshi wake wa kulinda amani waliokuwa kwenye eneo la mpaka wa Israeli na Syria linalopatika kwenye sehemu maarufu ya Golan baada ya wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa UN kujeruhiwa. Walinzi hao wa kulinda amani waliochini ya Umoja wa Mataifa UN walijeruhiwa baada ya kuzuka mapigano makali baina ya Jeshi la Syria na wapiganaji wa Upinzani ambao walikuwa wanashikilia eneo hilo la Golan.

Eneo la Golan ambalo linalindwa na Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa UN
Eneo la Golan ambalo linalindwa na Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa UN REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Kulinda Amani waliochini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa UN na kushika doria huko Golan waliojeruhiwa ni kutoka Ufilipino na India kitu ambacho kimezua maswali ya usalama ya wanajeshi hao.

Austria imeonekana kukerwa na kitendo cha kushiuhudiwa mapiganao makali kati ya Jeshi la Syria linalopambana na wapinzani kwa lengo la kukomboa maeneo yaliyochini ya utawala wa Upinzani kama ilivyokuwa Golan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria Michael Spindelegger amempigia simu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akimfahamisha awaondoe wanajeshi wao waliopo huko Golan kutokana na usalama wao kuwa hatarini.

Spindelegger amesema wanataka wanajeshi wao 377 waliopo eneo hilo la mpaka wa Israeli na Syria wanapaswa kuondoka kujiepusha na machafuko zaidi ambayo yanaweza yakatokea kipindi hiki jeshi la Damascus linapambana na wapinzani.

Katibu Mkuu Ban ameonekana kuguswa na tamko la Serikali ya Austria na kwa sasa wanaangalia ni kwa namna gani wanaweza kupata wanajeshi wengine ili wachukue nafasi ya walinzi hao wa amani 377.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban, Martin Nesirky amekiri Kiongozi huyo kusikitisha na kilichotokea na kusababisha kujeruhiwa kwa walinzi wa amani wawili ambao wamesaidia kuweka utulivu huko Golan.

Jeshi la Serikali ya Syria linalomtii Rais Bashar Al Assad lilifanikiwa kuchukua utawala wa eneo la Golan linalopata ulinzi kutoka Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa UN lililokuwa linashikiliwa na Wapiganaji wa Upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.