Pata taarifa kuu
PALESTINA

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliapisha Baraza Jipya la Mawaziri chini ya Waziri Mkuu Rami Hamdallah

Baraza Jipya la Mawaziri nchini Palestina limeapishwa likiwa na Mawaziri ishirini na wanne wakiwa chini ya Waziri Mkuu Rami Hamdallah ili lianze majukumu ya kuwahudumia wananchi.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas akizungumza na Mawaziri 24 wa Baraza lake Jipya
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas akizungumza na Mawaziri 24 wa Baraza lake Jipya
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ndiye amewaapisha mawaziri hao ishirini na wanne na kusema hiyo ni serikali yake aliyoiamini na itaweza kuwalinda wananchi na kuwatumikia ipasavyo.

Kiongozi huyo wa Mamlaka ya Palestina amesema serikali hiyo mpya itafanyakazi kwa nguvu na umahiri wa hali ya juu kuhakikisha wanatekeleza mahitaji ya wananchi katika muda mfupi ujao.

Serikali hiyo mpya ya Abbas ilichelewa kutajwa na hatimaye kuapishwa kutokana na kutokuwa na Waziri Mkuu hadi pale alipochaguliwa Hamdallah ambaye sasa atakuwa Kiongozi wa shughuli za serikali.

Mabadiliko ya Serikali yamekuja kutokana na uwepo wa kutokuelewana baina ya Rais Abbas na aliyekuwa Waziri Mkuu Salam Fayyad aliyeamua kujiuzulu mwezi Aprili na hivyo Hamdallah kuchukua nafasi hiyo kwa muda.

Waziri Mkuu Hamdallah amewaondoa hofu wananchi wa Palestina na kuwataka kutoa ushirikiano wa dhati kwa serikali mpya anayoiongoza ili iweze kufanikisha malengo yake ya kuijenga nchi hiyo.

Hamdallah amesema wananchi ndiyo wanaweza wakafanya kazi ya Serikali ikawa rahisi iwapo watawapa ushirikiano na kuondoa tofauti zilizopo baina ya Fattah na Hamas ambao wamekuwa wakivutana mara kwa mara.

Serikali mpya ya Mamlaka ya Palestina inatarajiwa kukabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha inashiriki kwenye mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu Mashariki ya Kati na jirani zao wa Israeli yanayosimamiwa na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.