Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI

Korea Kaskazini na Kusini zakubaliana kufanya mazungumzo juu ya eneo la Ukanda wa Viwanda wa Kaesong

Korea Kaskzani na Korea Kusini zimekubaliana kwa pamoja kufanya mazungumzo rasmi kwa mara ya kwanza ambayo yatajiegemeza kuangalia masuala ya kibiashara yatakayojiegemeza zaidi katika eneo la kiwanda cha Kaesong linalomilikiwa kwa pamoja na nchi hizo jirani. Uamuzi huo umefikiwa baada ya Korea Kaskazini kutuma ombi kwa jirani zao wa Korea Kusini kufanya mazungumzo ili kupata hatima juu ya eneo hilo la Ukanda wa Viwanda linalomilikiwa na mataifa hayo uliofungwa baada ya kuzuka hali ya kutoelewana.

Ukanda wa Viwanda unaomilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Korea Kaskazini na Korea Kusini la Kaesong.
Ukanda wa Viwanda unaomilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Korea Kaskazini na Korea Kusini la Kaesong. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Ukanda wa Viwanda wa Kaesong ilifungwa huku Korea Kaskazini ikiwafukuza wafanyakazi wote kutoka Korea Kusini waliokuwa wanafanya shughuli zao katika eneo hilo kipindi ambacho nchi hizo zilikuwa zinataka kuingia vitani.

Kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 2004 na kuwa kitovu kikubwa cha pande hizo mbili kutapa faida kubwa kutokana na biashara inayofanyika huku mwezi April Korea Kaskazini nayo ikaamua kuondoa wafanyakazi wake 53,000.

Korea Kusini imepokea kwa mikono miwili kwa pendekezo la kufanyika mazungumzo hayo yenye lengo la kuhakikisha suala la biashara baina ya nchi hizo mbili linarejea kama ilivyokuwa awali ili kuepukana na athari za kuzorota kwa uchumi katika nchi hizo.

Wizara ya inayoshughulikia masuala ya Muungano wa nchi hizo pili ya Korea Kusini imesema pendekezo hilo ni zuri na kwa sasa wanajiandaa kuhakikisha wanapanga tarehe ya kufanyika kwa mazungumzo hayo pamoja na agenda zitakazojadili baina ya nchi hizo mbili.

Haya yanaweza yakawa mazungumzo ya kwanza baina ya Seoul na Pyongyang tangu Korea Kusini iwatuhumu jirani zao wa Korea Kaskazini kuizamisha meli yao ya kivita mwezi Machi mwaka 2010 na kugharimu maisha ya watu 46.

Korea Kaskazini na Korea Kusini almanusura ziingia vitani kutokana na serikali ya Pyongyang kukerwa na hatua ya Seoul kufanya mazoezi ya kijeshi na Marekani ambayo yaliaminika kuwa sehemu ya uchokozi.

Hatua hiyo iliisukuma Korea Kaskazini kutoa kitisho cha kushambulia nchi za Korea Kusini, Japan na kambi zote za Marekani zinazopatikana kwenye eneo la Peninsula wakishinikiza kuondolewa vikwazo kutokana na kuendelea kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.