Pata taarifa kuu
UJERUMANI-AUSTRIA-JAMHURI YA CZECH

Watu 12 wamepoteza maisha Barani Ulaya kipindi hiki mafuriko yakiendelea kuwa kitisho kwa Majiji ya Ujerumani

Mafuriko yaliyozikumba nchi zinazopatikana Ulaya Kati zimeendelea kukumbwa na madhara makubwa zaidi kipindi kukiwa na taariaf mvua inayoendelea kunyesha inaweza ikaongeza kiwango cha maji.

Maji yaliyofurika kwenye mito Barani Ulaya yamesababisha mafuriko kwenye Majiji mengi kipindi hiki mvua unaendelea kunyesha
Maji yaliyofurika kwenye mito Barani Ulaya yamesababisha mafuriko kwenye Majiji mengi kipindi hiki mvua unaendelea kunyesha
Matangazo ya kibiashara

Majiji ambayo yanatajwa kuathirika zaidi na ongezeko hilo kubwa la maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ni pamoja na ile inayopatikana katika nchi ya Ujerumani, jamhuri ya Czech na Austria.

Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mafuriko hayo mabaya kutokea katika eneo la Ulaya Kati baada ya hali kama hiyo kushuhudiwa katika nchi hizo mwaka 2002.

Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mafuriko hayo imefikia kumi na wawili huku watu wengine wawili wakiwa hawajulikani walipo na juhudi za kuwasaka zingali zinaendelea.

Serikali za Ujerumani, Jamhuri ya Czech na Austria zimeendelea kutoa misaada kwa wale ambao wameathiriwa na mafuriko hayo huku wakiahidi kuendelea kukabiliana na hali hiyo ili kurejesha mambo kama awali.

Mafuriko hayo yamekuwa yakihusishwa na kufurika kwa mito kwenye mataifa ya Ulaya Kati kitu ambacho kimechangia kupasuka kwa kingo zake na hivyo majia kuanza kusambaa ovyo.

Mto Elbe ndiyo unatajwa kuchangia mafuriko katika nchi ya Ujerumu baada ya kingo zake kupasuka huku kukiwa na taarifa hatab Mto mkubwa wa Danube umejaa maji kitu ambacho kinaongeza hofu ya kutokea mafuriko zaidi.

Wananchi wametakiwa kuondoka katika maeneo yote ambayo yametajwa huenda yakakumbwa na mafuriko kutokana na kuwa karibu na mito iliyofurika maji kipindi hiki mvua zinaendelea kunyesha kwa nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.