Pata taarifa kuu
NIGERIA

Serikali ya Nigeria imeyatangaza Makundi ya Wanamgambo wa Boko Haram na Ansaru kuwa ni ya kigaidi

Serikali ya Nigeria imetangaza rasmi hatua ya kuyajumuisha makundi ya Wanamgambo wa Boko Haram na Jama'atu Ansaru kuwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi pamoja na kupitisha sheria ya kupiga marufuku uwepo wa makundi ya aina hiyo nchini humo.

Wanamgambo wa Kundi la Boko Haram ambao kundi lao limetajwa kuwa la kigaidi na serikali ya Nigeria
Wanamgambo wa Kundi la Boko Haram ambao kundi lao limetajwa kuwa la kigaidi na serikali ya Nigeria Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ndiye ametangaza hatua hiyo ya kuyatambua makundi hayo kuwa ya kigaidi tamko ambalo limetangazwa kwente gazeti la serikali kuonesha limeridhiwa na linaaza kufanya kazi.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Rais Jonathan imesema kundi lolote ambalo linaendelea kuwa na misingi kama ya Boko Haram na Ansaru yatakuwa yanakwenda kinyume cha sheria ya kupambana na ugaidi nchini humo.

Serikali ya Nigeria imeweka wazi kabisa mtu au kikundi ambacho kitafanya mambo yoyote ambayo yatahusiana na makundi ya Boko Haram na Ansaru naye atajumuishwa kwenye makosa dhidi ya ugaidi.

Taarifa hiyo imesema makundi ya Boko Haram na Ansaru na hata wale watu wanaojihusisha na makundi hayo wakikamatwa watafikishwa mahakama na kuhukumiwa kwa sheria dhidi ya ugaidi na iwapo akikutwa na hatia atakumbana na kifungo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kupambana na Ugaidi nchini nigeria inasema mtu ambaye anakutwa na hatia ya kutenda makosa ya ugaidi anapaswa kuhukumiwa adhabu ya kifungo kisichokuwa chini ya miaka 20 jela.

Kundi la Boko Haram limekuwa likiendesha mapambano dhidi ya serikali likipinga uwepo wa elimu ya magharibi inayotolewa kwa wanafunzi wa taifa hilo huku wao wakitaka uwepo wa matumizi ya sharia.

Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 na linahusishwa na mauaji ya watu zaidi ya 3,600 wakiwemo watu wa vyombo vya usalama katika mashambulizi yaliyopangwa na kutekelezwa katika eneo la Kaskazini mwa Taifa hilo.

Tangazo hilo la kuyatambua makundi ya Boko Haram na Ansaru kuwa yakigaidi linakuja kipindi hiki serikali ikiwa imetangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya Yobe, Borno na Adamawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.