Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

UN yaliorodhesha kundi la Al Nusra nchini Syria kama kundi la kigaidi, baadhi wahoji ushiriki wake nchini humo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN hiyo jana limetangaza kuliongeza kundi la al Nusra la nchini Iraq lenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi. 

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura kuhusu Syria
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura kuhusu Syria UN Photo/Evan Schneider
Matangazo ya kibiashara

Kwenye kikao cha siku ya alhamisi, wajumbe wa baraza la Usalama wamekubaliana kwa kauli moja kuliorodhesha kundi hilo kati ya makundi ya kigaidi yanayolengwa na vikwazo vya umoja huo.

Katika maazimio yao, nchi wanachama zimewawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo ikiwemo kuzuia mali zao, kuwazuia kusafiri pamoja na vikwazo vya silaha.

Kundi la Al-Nusra limekuwa likipigana vita nchini Syria sambamba na wapiganaji wa jeshi huru la Syria hatua ambayo sasa UN inaona kundi hilo halifai kuendelea kuwasaidia waasi kwakuwa lina uhusiano na Al-Qaeda.

Hatua ya Umoja wa Mataifa kutangaza vikwazo dhidi ya kundi hilo, inakuja kufuatia kiongozi wake, Ayman al-Zawahri mwezi mmoja uliopita kutangaza hadharani kuwa kundi lake lina uhusiano wa karibu Al-Qaeda.

Nchi ya Marekani yenyewe ilishaliorodhesha kundi hilo kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa vita hivyo vitazidi kuwa vibaya zaidi kufuatia hatua ya Umoja wa Ulaya kuwaondolea vikwazo vya silaha waasi wa Syria kwakuwa silaha hizo pia zitaishia kwenye makundi ya kigaidi kama ya Al Nusra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.