Pata taarifa kuu
NIGERIA

Bunge nchini Nigeria lapitisha sheria kuzuia ndoa za watu wa jinsia moja

Wabunge nchini Nigeria wamepiga kura na kupitisha sheria inayokataza ndoa za watu wa jinsia moja na kwamba atakayepatikana na kosa hilo atakumbana na kifungo cha miaka 14 jela.  

Baadhi ya wanaharakati wa Nigeria wanaotetea ndoa za watu wa jinsia moja
Baadhi ya wanaharakati wa Nigeria wanaotetea ndoa za watu wa jinsia moja Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo ambayo pia iliungwa mkono na bunge la seneti imekataza pia uundaji wa makundi ama taasisi za kutetea wanandoa wa jinsia moja wala vitendo vya usagaji na ushoga.

Sheria hiyo ambayo ilipendekezwa na bunge la seneti mwaka 2011 sasa inatarajiwa kupelekwa kwa rais Goodluck Jonathan ambaye atatia saini na kisha kuanza kutumika kama sheria rasmi.

Sheria hiyo inasema ni kinyume cha sheria kwa mtu ama kikundi cha watu kutekeleza ndoa za jinsia moja wala usagaji na kwamba atakayepatikana na hatia ya kutenda kosa hilo atahukumiwa na kifungo cha kisichopungua miaka 10.

Sheria hiyo inapitishwa wakati huu ambao nchi ya Ufaransa siku ya Jumatano imeshuhudia kwa mara ya kwanza kukifungwa ndoa za watu wa jinsia moja.

Mataifa mengi barani Afrika yanapinga ndoa za watu wa jinsia moja huku baadhi yao zikipitisha sheria kama ya Nigeria kuzuia uwepo wa makundi wala taasisi ambazo zitakuwa zinajihusisha na kutete watu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.