Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-NIGER

Kundi la MUJAO la nchini Niger, latishia kushambulia maslahi ya taifa la Ufaransa popote duniani na nchi yoyote itakayoingilia.

Baada ya Kundi la kigaidi linaloongozwa na raia wa Algeria Mokhtar Belmokhtar kumedai kutekeleza mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga na kuua watu ishirini limetishia kutekeleza mashambulizi zaidi nchini humo na nchi nyingine itakayoinuka kinyume na kundi hilo.

Moja kati ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la MUJAO ambalo limetishia kushamulia maslahi ya Ufaransa na taifa lolote litakalopinga kundi hilo nchini Mali
Moja kati ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la MUJAO ambalo limetishia kushamulia maslahi ya Ufaransa na taifa lolote litakalopinga kundi hilo nchini Mali AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo amekiri kuendeleza mashambulizi zaidi taarifa ambayo imepatikana kupitia mtandao wa kundi hilo la kigaidi na kutishia taifa la Ufaransa na taifa lingine lolote litakalothubutu kuingilia vita vya waislamu hao wenye msimamo mkali nchini Mali.

Watu zaidi ya ishirini wanakadiriwa kuuawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa muhanga nchini Niger kwenye machimbo ya Uranium yanayomilikiwa na kampuni ya Ufaransa, shambulio la ulipizaji kisasi kufuatia majeshi ya Ufaransa kuvamia kaskazini mwa Mali.

Msemaji wa kundi la MUJAO la nchini Niger, Abu Walid Sahraoui amekiri kundi lake kuhusika na shambulio hilo na kuongeza kuwa litaendelea kushambulia maslahi ya taifa la Ufaransa popote duniani.

Oumaru Garba ni mkuu wa operesheni ya kijeshi kwenye eneo la Arlit ambako shambulio hilo limetekelezwa, amesema kuwa juhudi za makundi ya wapiganaji wa kiislamu kuharibu usalama hazitafua dafu.

Wanaharakati nchini humo wanalaani shambulio hilo na kuitaka serikali kuzidisha usalama kwenye maeneo ya mpakani na nchi ya mali kwakuwa wapiganaji hao ndiko wanakojipenyeza kutekeleza mashambulio hayo.

Kundi la MUJAO limefurushwa kaskazini mwa Mali baada ya kushikilia maeneo hayo kwa miezi kadhaa kabla ya uvamizi wa majeshi ya Ufaransa na vile vikosi vya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.