Pata taarifa kuu
SYRIA

Takribani waasi 56 wauwawa katika shambulizi la wanajeshi wa Syria

Waasi wa Syria wapatao 56 wameuwawa usiku wa kuamkia leo baada ya jeshi la serikali kutekeleza mashambulizi zaidi ya anga kwenye ngome kuu ya wapiganaji wa Syria mjini Qusary, siku moja toka rais Bashar al-Asad asisitize kutong'atuka madarakani. 

Wanajeshi wa Syria
Wanajeshi wa Syria globalpost.com
Matangazo ya kibiashara

Taasisi ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria imesema mapigano hayo yamesababisha vifo vya waasi takribani 56 sita kati yao wakiwa wameuwawa leo Jumatatu na raia wanne akiwemo mwanamke.

Vita hiyo alianza jana Jumapili, wakati askari wa serikali wanaoungwa mkono na wapiganaji wa Hezbollah walipovamia mji wa Magharibi, kitovu cha harakati za kivita za miaka miwili nchini humo.

Mapigano hayo yamezua hofu ya mauaji na kuweka wingu kwenye juhudi za Marekani na Urusi za kuandaa mkutano wa amani wa kujadili ufumbuzi wa vita ya kisiasa nchini Syria.
 

Upinzani umekosoa hatua ya mashambulizi hayo ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mji huo ni muhimu kwa utawala wa Asad kwa kuwa unapakana na Lebanon ambako wapiganaji wa Hezbollah wanausaidia utawala wake.

Umoja wa nchi za Kiarabu umeitisha mkutano wa dharura Alhamisi ya wiki hii kujadili machafuko yanayoendelea nchini humo wakati huu ambapo nchi za Urusi na Umoja wa Mataifa zimekubaliana kuitisha mkutano wa kimataifa kujadili hali ya Syria.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.