Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yaondoa Makombora yake kabla ya Marekani na Korea Kusini hazijafanya mkutano wa kujadili Usalama wa Eneo la Peninsula

Serikali ya Korea Kaskazini imefikia uamuzi wa kuondoa makombora yake mawili katika Pwani yake ambayo yaliwekwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa majaribio licha ya Pyongyang na Korea Kusini kuendelea kutunishia misuli na kutishia kuwa tayari kuingia vitani. Pyongyang iliweka makombora yake hayo kuelekea nchini Korea Kusini ikiwa ni kujiandaa na mpango wake wa kuingia vitani na jirani zao hao wa Seoul ambao walikuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi kwa kushirikiana na Majeshi ya Marekani.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un akiwa akiangalia maeneo waliyoweka makombora yao ya kujilinda kabla ya kuondolewa
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un akiwa akiangalia maeneo waliyoweka makombora yao ya kujilinda kabla ya kuondolewa
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa Marekani ndiyo wamethibitisha hatua ya Korea Kaskazini kuondoa makombora yao hayo mawaili yaliyokuwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa majaribio kitu ambacho kinadhihirisha utulivu wa eneo la Peninsula umeanza kurejea.

Makombora hayo yameondolewa kipindi hiki ambacho Korea Kusini na Marekani zikijiandaa kufanya mkutano wao huko Washington ambapo miongoni mwa vita vitakavyojadiliwa ni pamoja na hali ya usalama katika Peninsula.

Korea Kaskazini ilifikia uamuzi wa kuweka makombora yake hayo mawili ya masafa marefu tayari kutokana na kuwa na lengo la kuzishambulia Korea Kusini, Japan pamoja na kambi za kijeshi za Marekani zilizokwenye eneo la Peninsula.

Pyongyang ilitishia kushambulia maeneo hayo baada ya Umoja wa Mataifa UN kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya taifa hilo mwezi Machi mwaka hu kutokana na nchi hiyo kuendelea kufanya majaribio ya zana zake za kinyuklia.

Marekani na Korea Kusini ziliingiwa na hofu kutokana na mkakati wa Korea Kaskazini kutaka kufanya majaribio ya makombora yake ya masafa ya kati na hivyo wakaanza kuchukua hatua za kujilinda kwa kuweka ngao maalum.

Marekani imeonekana kufurushwa na hatua ya Korea Kaskazini kuondoa makombora yake hayo mawili na kuelezahakuna kitisho tena cha kufanyika kwa majaribio ya silaha hizo za nyuklia.

Uamuzi huu wa Korea Kaskazini kuondoa makombora yake mawili katika mpaka wake na Korea Kusini umeonesha hatari ya kuzuka kwa vita katika eneo hilo la Peninsula na hali itazidi kuimarika ya kuonesha usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.