Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Waziri wa mambo ya nje wa Mali azuri nchini Algeria wakati Ufaransa ikianza kuyaondowa majeshi yake nchini Mali

Jeshi la Ufaransa ambalo limetangaza kuanza kuyaondowa majeshi yake nchini Mali, linaendelea na operesheni ya kupambana na wapiganji wa kundi la kiislam la Mujao (vuguvugu la Umoja kwa ajili ya Jihad Afrika Magharibi) karibu na mji wa Gao.Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Mali Hubert Coulibaly amewasili nchini algeria kwa ziara ya siku moja kujadili na viongozi wa nchi hiyo kuhusu swala la usalama.

waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Coulibaly,jijini Brusels Januari 17, mwaka  2013.
waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Coulibaly,jijini Brusels Januari 17, mwaka 2013. AFP PHOTO / JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema ziara yake hiyo inalenga kuzungumzia maswala yanayo yahusuyo mataifa hayo mawili ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano bora baina ya Algeria na Mali, na swala lihusulo amani na usalama wa dunia.

Algeria inachangia mpaka na Mali wenye umbali wa kilometa elfu moja na mia tatu ambapo jeshi la Ufaransa likishirikiana na majeshi ya Mali yalianzisha operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa makundi ya kiislam yenye mafungamano na kundi la Alqaeda kaskazini mwa Mali.

Hapo jana katika kipindi cha miezi mitatu jeshi la ufaransa limeanza kuyaondowa majeshi yake kaskazini mwa Mali ambapo wanashi zaidi ya mia moja wamereja nyumbani.

Kwa mujibu wa rais wa Ufaransa Francois Hollande, ifikapo mwezi Julay mwaka 2013 watasalia pekee nchini humo wanajeshi wasiopungua elfu mbili badala ya elfu nne waliopo kwa sasa. Mwezi Julay ndio mwezi ambao serikali ya Paris imelazimisha kwa Mali kuandaa uchaguzi wa rais na bunge.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.