Pata taarifa kuu
Korea-UN

Ban Ki Moon azionya Korea Kusini na Kaskazini kutumia busara katika kutanzua matatizo yao.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amewatolea wito viongozi wa Korea Kaskazini kuepusha kila njia zote za uchochezi, wakati serikali ya Seoul ikitangaza kwamba jirano yake Korea Kaskazini ikijiandaa kuendesha jaribio la nne la makombora ya masafa marefu.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki Moon amesema anawatolea wito pande zote mbili kutochukuwa hatuwa zozote ambazo zinaweza kuleta uchochezi. Ameyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje ya Uholanzi Frans Timmermans huku akiongea kwamba ni wito wa dharura na kwamba wanatakiwa kutumia busara katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliopo badala ya kutumia mabavu.

Ban ameendelea kusema kwamba jamuhuru ya kidemokrasia ya watu wa Korea haiwezi kuendelea kukakidi wito na mamlaka ya baraza la uslama la Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa.

Ikighadhabishwa kwa mara ya tena na mfumo mpya wa vikwazo vilivyopitishwa na Umoja wa Mataifa baada ya kufanya majaribio ya nyuklia Februari iliopita pamoja na mpango wa mazoezi yakijeshi ya pamoja unaoendelea kati ya kati ya Marekani na Korea Kusini, Korea ya Kaskazini imeongeza kauli za kichochezi.

Korea Kaskazini imeweka makombora hivi karibuni katika pwani yake na pia inaweza kufanya majaribio ya kurusha wiki hii katika jitihada kwa ajili ya maridhiano kutoka Washington, kwa mfano kuanzishwa bila masharti kwa mazungumzo juu ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.