Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa balozi mbalimbali na mashirika ya kimataifa juu ya usalama wao endapo mapigano yatazuka kati yake na Korea Kusini

Korea Kaskazini imezitaka balozi mbalimbali kuanza kuhamisha makazi yake nchini humo wakati huu ambapo tayari nchi hiyo imepeleka makombora yake katika Pwani ya Mashariki na kuzidisha hofu ya vita kwa majirani zao Korea Kusini.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Pyongyang imeonya haitahusika na kulinda usalama katika balozi za nje na mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini humo baada ya tarehe 10 ya mwezi huu endapo mapigano yatazuka.

Uingereza na Urusi ni miongoni mwa nchi za Ulaya zilizopewa barua kuhusiana na usalama wa balozi zao.

Kwa upande wake Marekani imesema haishangazwi na hatua hiyo kwani si ya kwanza kuchukuliwa na imeionya Pyongyang kuachana na vitisho hivyo.

Hofu ya kuibuka kwa vita imezidi kushika kasi baada ya Korea Kaskazini na Marekani kuendelea kutunishiana misuli kutokana na kila upande kuweka tayari silaha zake kwa ajili ya kujibu mashambulizi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ametoa wito kwa Pyongyang kuachana na mpango wake wa kutaka kuishambulia Korea Kusini na Marekanikwani hatua hiyo inaweza kikachangia kuzuka kwa vita na kuleta madhara makubwa zaidi.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.