Pata taarifa kuu
MYANMAR

Serikali ya Myanmar yaruhusu uchapishaji na usambazaji wa magazeti yanayomilikiwa na watu binafsi ikiwa ni miongo karibu mitatu tangu yaingie kitanzini

Serikali ya Myanmar imanza kuonesha kwa vitendo inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari baada ya kuruhusu kuchapishwa na kusambazwa kwa magazeti binafsi ambayo kwa miongo kadhaa yalikuwa kitanzini.

Wauzaji wa magazeti nchini Myanmar wakiwa na magazeti yaliyoruhusiwa kuuzwa baada ya kuwa kitanzini kwa miongo kadhaa
Wauzaji wa magazeti nchini Myanmar wakiwa na magazeti yaliyoruhusiwa kuuzwa baada ya kuwa kitanzini kwa miongo kadhaa
Matangazo ya kibiashara

Magazeti manne ambayo yalikuwa yanachambishwa na kusambazwa kila siku hatimaye yameshuhudiwa mitaani kwa mara nyingine ambayo ni pamoja na The Voice, The Golden Fresh Land, The Union na The Standard Time.

Uamuzi wa kuyafungulia magazeti hayo umekuja baada ya serikali ya kiraia kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari ufanyekazi yake tofauti na ilivyokuwa kwa serikali ya kijeshi iliyoongozwa kwa miongo zaidi ya miwili.

Sheria mpya ya Uhuru wa vyombo vya habari imekuja kuleta mageuzi kwenye sekta hiyo na sasa magazeti yatakuwa yakitolewa kama ilivyokuwa awali na hii ni sehemu ya kurejesha demokrasia nchini Myanmar.

Wananchi wengi wamepokea kwa furaha hatua hiyo ya kurejea tena kwa magazeti hayo yanayomilikiwa na watu binafsi huku kwenye maeneo ya kuuzia magazeti mamia ya wananchi wameonekana wakinunua magazeti hayo.

Sheria hiyo mpya imeyataka makampuni binafsi kuhakikisha yanakuwa na magazeti ya kila siku na kuachana na mfumo wa zamani wa kutoa magezeti kwa juma mara moja kabla ya kuingia kitanzini.

Mhariri wa Gazeti la The Voice Aung Soe amesema wamefanyakazi kwa kipindi cha miezi sita ili kuhakikisha wanaweza kuingia kwenye mfumo wa kutoa gazeti lao kila siku badala ya wiki mara moja kama awali.

Tangu Utawala wa Kiraia kuingia madarakani mwaka 2011 na kumaliza utawala wa kijeshi uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili na kusababisha nchini Myanmar kuwekewa vikwazo kumekuwa na mabadiliko mengi yakilenga kurejesha demokrasia na kuheshimu utawala wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.